Afisa Usambazaji wa Global, Kefa Masaga, akigawa vipeperushi vya Shinda Nyumba katika mitaa ya Ubungo, Riverside.
BAHATI nasibu ya Shinda Nyumba inayoendelea chini ya Kampuni la Global Publishers wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Championi, Ijumaa, Amani na Risasi, inazidi kukimbiza ambapo watu mbalimbali, waume kwa wake wanaendelea kujitokeza kwa kujaza kuponi ili kujitengenezea nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali kila mwezi zikiwemo pikipiki na simu za kisasa (smart phones) hatimaye kujishindia nyumba katika droo kubwa itakayochezeshwa hapo baadaye.
Ofisa Usambazaji wa Global Publishers, Jimmy Haroub, akiwa na dereva bodaboda wa Riverside Ubungo baada ya kujaza kuponi.Naftali Muwayamamo, mkazi wa Ubungo akijaza kuponi.Living Patrice, mkazi wa Moshi Mjini akijaza kuponi.Lucy Mwalemba, mkazi wa Ubungo akijaza kuponi.Kefa Masaga akigawa vipeperushi vya Shinda Nyumba mitaa ya Riverside Ubungo.Jimmy Haroub akimshuhudia Richard Timoth mkazi wa Riverside akija kuponi ya Shinda Nyumba.Kefa akimsaidia Salma Ally mkazi wa Ubungo kujaza kuponi.…Akiwapa maelekezo wasomaji wa magazeti ya Global jinsi ya kushiriki Shinda Nyumba.…Akiwa na wasomaji wa magazeti ya Global akiwaelekeza namna ya kujaza kuponi.Jimmy akimsaidia kujaza kuponi Rehema Muhanji, mkazi wa Manzese.
Baaada ya kuzunguka katika maeneo mengi jijini Dar, timu ya promoseni ya bahati nasibu hiyo leo ilitinga mitaa ya Riverside-Ubungo ambako watu mbalimbali walijitokeza kwa wingi na kujaza kuponi huku kila mmoja akionyesha wazi kwa vitendo kuwa amedhamiria kutwaa mjengo, ambayo ndiyo zawadi kubwa ya shindano hilo kwa kujaza kuponi.