
MWANAMAMA wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel anasema kuwa, watu wengi ambao ni wabaya ndiyo ambao wanamzunguka mtu na kila wakati anacheka nao kwa kuwaamini bila kujua ndiyo watakaommaliza.
Aunt anasema kuwa, amejifunza vitu vingi mno kupitia maisha yake ambayo ameishi kuwa mara nyingi watu wa karibu ndiyo wanawageuka siku hadi siku hivyo ni muhimu kubadilika.
“Mimi niliwahi kuambiwa kuwa mtu ambaye anakuumiza hatoki mbali kwa sababu mtu wa mbali hawezi kukumaliza,bali wa karibu yako na wengi wao wanakuwa ni marafiki zetu wa kila siku hivyo tuchunge sana tunaowachekea,” anasema Aunt; mama wa watoto wawili.