
Na MWANDISHI WETU| RISASI MCHANGANYIKO| HABARI
MTANDAO : Mrembo Alhuda Njoroge, maarufu kama Huddah Monroe, mwanamitindo na mjasiriamali kutoka Kenya, nusura apoteza maisha wakati zoezi lake la kuongeza ukubwa wa matiti lililofanyika nchini Marekani kumletea shida.
Kwa mujibu wa maelezo aliyoandika katika akaunti yake kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram, Huddah alisema kama siyo msaada wa madaktari bingwa wa kliniki ya Beverly Hills, huenda angepoteza maisha.

“Nilipata matatizo kidogo kutokana na upasuaji niliofanyiwa hapo awali na lazima niwashukuru sana madaktari kwa kazi nzuri ambayo wameifanya kwangu. Ninawashukuru sana, ningeweza kufa kwa kweli, ila sasa niko poa,” aliandika mshiriki huyo wa Big Brother Africa, 2013.
Katika andiko lake hilo, aliwashukuru madaktari kutoka kituo hicho, Beverly Hills Surgery Group, moja kati ya kliniki zinazoaminiwa zaidi kwa ubora wa kazi zao, wakiaminika kurekebisha makosa makubwa yanayoweza kuwa yamefanywa na wengine.
Wakati akiwa katika Shindano la Big Brother 2013, ‘clip’ kadhaa zilivuja, zikionyesha msichana huyo kuwa na matiti yenye umbile dogo, inayosemekana haikumfurahisha, hivyo kufikia uamuzi wa kutaka kuongeza ukubwa wa viungo hivyo muhimu.