×

Prof. Mkumbo Aitaka Dawasco Kuongeza Kasi Utoaji Huduma jijini Dar

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo akizungumza na baadhi ya uongozi wa mamlaka hiyo.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo ameitaka Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASCO), kuongeza kasi ya usambazaji wa huduma ya maji kwa wananchi ili kufikia malengo ya serikali.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo wakati akiongea na uongozi wa mamlaka hizo mbili leo jijini Dar es Salaam. Profesa Mkumbo amesema kuwa licha ya ongezeko la upatikanaji wa maji, zipo changamoto kubwa kwa wananchi kutofikiwa na huduma, hivyo ni lazima mamlaka husika kuongeza kasi ya usambazaji wa miundombinu ya maji.
Baadhi viongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASCO) wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea.
Mkumbo ametoa rai kwa wateja wote wa Dawasco zikiwemo taasisi za umma, kutii agizo la Rais Magufuli la kulipia huduma wanazopatiwa ili kuziwesha mamlaka husika kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa uzalishaji wa maji umeongezeka kutoka lita za ujazo wa mita 160 milioni kwa siku hadi kufikia lita za ujazo mita 271milioni kwa siku ambazo ni sawa na asilimia 100.37% ya lengo la upatikanaji wa maji ambalo ni lita 270 milioni kwa siku.
  
Katika kuhakikisha inafikia azma ya kuongeza kasi ya usambazaji wa huduma ya maji kwa wananchi Dawasco inaendesha kampeni ijulikanayo.
 “Mama Tua Ndoo ya Maji Kichwani Ndani ya Siku 90” ikiwa na lengo la kuwaunganisha na huduma ya maji wateja takribani 151,000. Kampeni hiyo ilianza Aprili, Mosi na inatarajia kumalizika Juni 30, 2017.

Leave a Comment