×

Rungwe Aomba Kukutana na Magufuli Amshauri

Aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Chauma, Hashimu Rungwe akiwa ndani ya ofisi ya Global Publishers leo.
Mhariri wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli (kulia)  akimtambulisha Hashimu Rungwe wakati wa mahojiano na Global TV Online.
Hashimu Rungwe akiwa katika pozi wakati wa mahojiano.
Wafanyakazi wa Global Publishers wakiwa katika picha ya pamoja na Hashimu Rungwe.

 

…Wakiagana na Hashimu Rungwe.
Hashimu Rungwe akiwa ndani ya ndinga yake.

Picha : Brighton Masalu

Mwenyekiti wa Chama Cha Umma (Chauma), Hashim Rungwe amesema ingefaa Rais Dk. John Magufuli akawaalika viongozi wa siasa ili waweze kumpa ushauri wa kiuchumi na kisiasa ili nchi iweze kupiga hatua kimaendeleo.

Akizungumza na Global TV leo, Rungwe alisema kuna mambo ya msingi ambayo serikali inakosea lakini wao kama wanasiasa wanashindwa kupata nafasi ya kumshauri rais wa nchi.

“Yapo mambo mazito ambayo tungeweza kumshauri rais lakini hajataka kukutana na sisi viongozi wa siasa. Natoa ushauri akutane na sisi kwani kuna mengi ya kumweleza kama vile nchi kuwa na ndege za kumwagilia mashamba badala ya hizo za aibiria na mambo mengine mengi ya kiuchumi,” alisema Rungwe.

Akifafanua zaidi kiongozi huyo ambaye aliwahi kuwa mgombea urais mwaka 2015 alisema, taasisi ya urais inafaa kupewa ushauri ili iwatumie vizuri watu wenye taaluma maana hata Yesu na Mtume Muhammadi walifanikiwa baada ya kuwa na jopo la washauri wao.

Leave a Comment