×

Mfumuko wa Bei Waongezeka kwa Asilimia 0.5

Mfumuko wa bei wa mwezi kwa Aprili mwaka huu, unaopimwa kwa kila mwezi, umeongezeka kwa asilimia 0.5 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 1.4 ilivyokuwa kwa mwezi Machi 2017.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo, akiongea na waandishi wa habari na kufafanua kwamba pamoja na ongezeko hilo bei zimeongezeka hadi asilimia 109.04 kwa mwezi Aprili kutoka 108.44 mwezi Machi mwaka huu.

Amesema ongezeko hilo limechangiwa na ongezeko la bei za bidhaa za vyakula ambavyo ni mahindi, kwa asilimia 4.8, unga wa mahindi kwa asilimia 7.1, choroko kwa aslimia 6.5, viazi mviringo 4.0%, nyanya 7.8%, nazi kwa asilimia 6.9 na mihogo  kwa 5.9 pamoja na vitunguu kwa 3.5.

Alisema kwamba thamani ya Shilingi ya tanzania hupima badiliko la uwezo katika kununua bidhaa na huduma zilezile za mlaji ambazo Shilingi ingeweza kununua katika vipindi tofauti.

Na Denis Mtima|GPL

Leave a Comment