×

PICHAZ: Watoto Wawili Ajali ya Karatu Wazikwa, Mmoja Asafirishwa Tanga

WATOTO wawili kati ya 32 waliofariki kwa ajali ya gari Jumamosi iliyopita wilayani Karatu walizikwa jana huku mmoja akisafirishwa na kupelekwa mkoani Tanga kwa ajili ya mazishi baada ya kuagwa kitaifa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

Mwili wa Eliapenda Eliud ukishushwa kwenye gari kuelekea kanisani.

Baada ya kuagwa kitaifa ambapo Makamu wa Rais, Bi Samia Suluhu aliwaongoza maelfu ya Watanzania kuwaaga watoto hao, walimu wawili na dereva mmoja, miili ya watoto hao watatu ilipelekwa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini ambapo misa maalum ya kuwaaga.

Baada ya kuagwa kanisani hapo, watoto wawili ambao ni Ruth Ndemno Piniel wa kike mwenye umri wa miaka 14 na Eliapenda Eliud Shila wa kike mwenye umri wa miaka 13, walizikwa katika makaburi ya kanisa hilo Mtaa wa Olasiti, Arusha.

Mwili wa mtoto mwingine wa tatu, Witness Philemon Laizer, wa kike mwenye umri wa miaka 14, ulichukuliwa na ndugu zake na kusafirishwa kwenda nyumbani kwao mkoani Tanga ambako mazishi yanatarajiwa kufanyika leo.

Mzazi wa Witness Philemon (wa pili kulia) ambaye mwili wake ulisafirishwa na kupelekwa nyumbani kwao Tanga kwa mazishi.

Mzazi wa marehemu Eliapenda Eliudi (aliyevaa mavazi meupe) akiwa katika ibaada ya kumuaga mwanaye.

Ibada ya kuaga miili ya marehemu ikiendelea kanisani.

Baba mzazi wa Ruth Ndemno, Mzee Ndemno (wa kanza kushoto) wakati wa ibada ya kuaga miili ya watoto hao.

Taarifa zilizopatikana kutoka kwa ndugu wa marehemu Ruth zilieleza kuwa mama yake mzazi naye alishatangulia mbele za haki. 

Ndugu wakiaga miili ya marehemu.

Ndugu na waombolezaji wakielekea makaburini.

Eneo la makaburi ambapo miili hiyo ilizikwa.

Jeneza likiingizwa kaburini.

Miili ya watoto, Ruth Ndemno Piniel na Eliapenda Eliud Shila ikiwa kaburini.

Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu wakijumuika wakati wa mazishi.

PICHA NA HILALY DAUDI | GLOBAL PUBLISHERS– ARUSHA

Full Video: Majeneza 35 ya Wanafunzi Yakishushwa Kwenye Gari Arusha

Leave a Comment