×

Yanga Yawaahidi Mambo Mazuri Wachezaji Wake

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa.

Sweetbert Lukonge Championi Jumatano | Habari

KATIBU Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa ametaka wachezaji wa timu hiyo kuendelea kupambana uwanjani katika mechi zao zote zilizobakia ili kuhakikisha wanatetea ubingwa wao.

Mkwasa aliyasema hayo baada ya kuridhishwa kiwango cha juu walichoonyesha wachezaji wa timu hiyo katika mechi dhidi ya Prisons.

Akizungumza na Championi Jumatano, Mkwasa alisema kuwa hivi sasa uongozi unapambana vilivyo kuhakikisha unaimarisha hali ya kiuchumi klabu hapo hivyo anaamini kabisa baada ya muda mfupi mambo yatakuwa sawa.

“Nawapongeza wachezaji kwa kupambana vilivyo uwanjani ili kuhakikisha wanalinda heshima ya klabu yetu, japokuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za hapa na pale.

“Hata hivyo, niwaombe tu waendelee kupambana mwanzo katika mechi zetu zote zilizobakia na wasiwe na wasiwasi mambo yatakuwa mazuri tu na hizo changamoto zinazowakabili hivi sasa zitaisha tu,” alisema Mkwasa.

Leave a Comment