×

GlobalNewsAlert: Lita 6,694 za Kemikali za Kutengenezea Dawa za Kulevya Zakamatwa Dar

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kudhibiti dawa za kulevya, Rodgers Sianga.

DAR ES SALAAM: Kamishna wa Mamlaka ya Kupambana na Kuzuia Dawa za Kulevya nchini, Rogers Sianga amesema wamekamata kiasi cha lita 6,694 za kemikali bashirifu zinazoweza kutengeneza dawa za kulevya jijini Dar es Salaam.

Kamishna Msaidizi wa Ukaguzi na Sayansi ya Jinai, Bertha Mamuya akizungumza na wanahabari.

Mlimzi wa eneo hilo.

Baadhi ya makopo yenye kemikali.

Maboksi na chupa zenye kemikali.

Nje ya jengo hilo.

Akizungumza mapema leo baada ya kufanya oparesheni maalum iliyofanyika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, Sianga amesema kemikali hiyo imekamatwa katika Mtaa wa Kipepeo eneo la Mwenge jijini hapa.

Aidha amesema pia wamebaini kuwepo kwa maghala mengine yaliyopo Bagamoyo mkoani Pwani na Moshi mkoani Kilimanjaro.

PICHA NA SIFAEL PAUL | GLOBAL PUBLISHERS

=======================================================================

Leave a Comment