
IKULU, DAR: Rais Magufuli amemuapisha Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Bi. Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, leo Juni 6, 2017 na kumkabidhi Ilani ya CCM.
Baada ya kumuapisha, Rais Magefuli alipata fursa ya kumzungumza kuhusu uteuzi huo.
“Mimi huwa siteui watu hivi hivi, naangalia uwezo wa mtu, wewe nimekuchunguza na nimejiridhisha kuwa una uwezo wa kuwatumikia wananchi.
“Mimi nampongeza sana Mama Anna, ni mstaarabu, msomi mzuri na najua kwa nafasi niliyomteua atafanya kazi vizuri,
“Wengine wanasema nilikataa kuteua wapinzani, wajiulize nilizungumza hayo nikiwa wapi, mimi siwezi kuteua mbunge wa upinzani, maendeleo hayana chama, mama Anna nenda kachape kazi, amesema Rais Magufuli.
Baada ya kuapishwa Mghwira amesema;
“Ninasema hii ni heshima kwa Taifa letu, ni heshima kwa umoja wa nchi yetu, ni heshima kwa siasa za umoja wa nchi yetu.
“Kumekuwa na minong’ono mingi sana kuwa Rais analeta nini, kuteua watu wanaitwa wapinzani, mimi sio mpinzani wa maendeleo,” alisema Anna Mghwira.