OVER ZE WEEKEND
ZIKIWA zimesalia wiki kadhaa kuelekea Sikukuu ya Idd Mosi, imefahamika kuwa, Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar unatarajia kushusha sapraizi ya kimataifa ambayo haijawahi kufanyika Tanzania.
Akizungumza na Over Ze Weekend, Mratibu na Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa hadi sasa wakali watakaotoa shoo hiyo ni wengi na wameshajulikana lakini sapraizi ni kitu pekee kinachosubiriwa kwa hamu hivi sasa.
BONGO FLEVA
”Kwa upande wa Bongo Fleva imeshajulikana tutakuwa na wasanii kibao akiwemo Mr Blue ambaye anakamata vilivyo na vibao vyake matata kama vile Pesa, Mboga Saba, Baki Na Mimi na vingine vingi.
“Pia tutakuwa na kundi hatari kunako Muziki wa Asili la Makhirikhiri kutoka Tanzania ambao nao ni habari nyingine kwa sasa ukizungumzia burudani kwa watoto na wakubwa kwa hiyo tutakuwa nao kuanzia burudani ya watoto itakayoanza asubuhi ya saa mbili hadi saa 12:30 jioni na pia usiku.
ZANZIBAR STARS NAYO NDANI
Mbizo aliongeza kuwa burudani ya kibabe itaanza rasmi saa 2:00 usiku kwa wakali kibao kutumbuiza huku kundi kongwe linalosumbua mjini kwa sasa, Zanzibar Stars likipagawisha vilivyo.
“Zanzibar Stars ni baba la mababa na mama la mamama. Limerudi tena likiwa na wakongwe wengi wanaoijua Taarab hasa! Mashabiki wa muziki huu wa Mwambao waje kwa wingi kupata burudani ya aina yake kutoka kwa wakali kama Sabaha Muchacho, Zubeda Mlamali, Ally Jay, Mosi Suleimani, Jokha Kassim na wengine weeengi bila kumsahau fundi wa kinanda, Ally Jay.
TUDOKEZEE BASI SAPRAIZI HIYOOO!
Mbizo alidokeza kidogo tu sapraizi hiyo itakavyokuwa ndani ya Dar Live na kusema kuwa haijawahi kutokea Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla tangu Dar Live ianzishwe.
“Itakuwa ni zaidi ya shoo za akina Chris Brown, Lil Wayne, Drake, Nicki Minaj na wengine huko mbele wanavyozifanya zikiwa na sapraizi. Kama mtakumbuka Dar live pekee iliwahi kufanya sapraizi kubwa ya kimataifa kwa kumshusha Diamond na helikopta Dar Live na kupiga bonge moja la shoo la kihistoria ambalo bado ni gumzo hadi leo. Sasa mashabiki mjiandae na hii ya safari hii Dar Live inaliamsha tena dude tena ni zaidi ya hiyo ya helikopta,” alisema Mbizo.
MTONYO JE?
Mbizo alihitimisha kwa kuweka wazi kiingilio siku hiyo kuwa burudani kwa watoto itakuwa shilingi 3,000 ambapo watapata burudani kabambe kutoka kwa kundi la sarakasi lisilo na mpinzani Afrika Mashariki la Wakali Dancers pamoja na michezo kibao kwa watoto kama vile kuogelea, kubembea, kuteleza, bembea na mingine mingi huku burudani kwa wakubwa ikiwa kwa mtonyo wa buku saba (7,000) tu getini na watoto kiduuuuchu yaani buku tatu tu (3,000),” alimaliza Mbizo.