
MSANII wa filamu za Kibongo, Ester Kiama anadaiwa kupangishiwa mjengo na mwanaume ambaye ni mume wa mtu aliyemhamisha kutoka Kijitonyama alikokuwa anaishi na kumwamishia Mbezi Beach.
Chanzo makini kilieleza kuwa kwa sasa Ester anaishi kwenye nyumba nzima yenye hadhi tofauti na alikokuwa akiishi mwanzo ambapo amelipiwa kodi ya mwaka mzima na mwanaume huyo.

Risasi Jumamosi lilimtafuta Ester ili kujibu tuhuma hizo na alipopatikana alikiri kuhamia Mbezi Beach kwenye nyumba nyingine nzima lakini alipinga suala la kupangishiwa na mwanaume.
“Ninaishi Mbezi Beach kwa sasa ambako nimehamia hivi karibuni, habari za kwamba nimelipiwa kodi na mwanaume ni uongo, nimejilipia mwenyewe,” alisema Ester.

(Stori: Gladness Mallya, Risasi Jumamosi)