-

Marehemu Chiku aliyefariki jana katika Hospitali ya Amana jijini Dar 
Waombolezaji na ndugu wakilisawazisha kaburi la marehemu Chiku aliyefariki jana katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam wakati akijifungua. Mtoto wake pia aliyekuwa tumboni alifariki. 
Mzee Yusufu akiongoza waombolezaji kumwombea dua marehemu mkewe, Chiku. 
Mzee Yusuf (wa kwanza kushoto) akiingia kaburini kuupokea mwili wa mkewe, Chiku.

-

- Maziko yakiendelea.

- Mzee Yusuf akiwa katika masikitiko makubwa.

- Waombolezaji mbalimbali waliofika katika mazishi hayo.

- Jeneza la mwili wa marehemu likiingizwa katika makaburi ya Kisutu mchana wa leo.

- Mzee Yusufu akiwa amebeba mwili wa mtoto wake aliyefariki.


- Safari ya kuelekea makaburi ya Kisutu ikianzia nyumbani kwa marehemu.

- Mmoja wa waombolezaji akisoma kaswida.

- Mzee Yusuf akisaidiwa kuingia katika makaburi ya Kisutu.



MAMIA ya waombolezaji leo wamemzika marehemu Chiku Hamisi aliyekuwa mke wa mwimbaji taarab aliyestaafu na kumrudia Muumba wake, Ustaadhi Mzee Yusuf. Chiku aliyezikwa kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar leo mchana, alifariki dunia katika Hospitali ya Amana jijini Dar Jumamosi jioni ambapo alikwenda kujifungua.
Chiku alipoteza maisha akisaidiwa na wauguzi kujifungua kwa njia ya upasuaji ambapo mwanaye aliyekuwa tumboni alifariki pia.
Shughuli za msiba na mazishi zilianzia nyumbani hapo Kariakoo Mtaa wa Amani na Livingstone ambapo mwili ulitolewa nyumbani hapo na kwenda kuswaliwa kwenye msikiti wa Manyema.
Baada ya suala mwili ulipelekwa makaburi ya Kisutu jijini hapa.
Katika mazishi hayo Mzee Yusuf alishindwa kuzungumza chochote baada ya kuishiwa nguvu ambapo aliondolewa makaburini hapo kwa msaada wa waombolezaji.
Na Richard Bukos/GPL