×

Dar: Mwanafunzi Ajirusha Toka Ghorofa ya Nne Hadi Chini (VIDEO)

Mtoto anayedhaniwa kuwa ni Mwanafunzi wa  Shule ya DYCCC iliyopo Chang’ombe karibu na Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam amenusurika kifo baada ya kujirusha kutoka ghorofa ya nne mpaka chini.
Taarifa zisizo rasmi zimeeleza kuwa chanzo cha tukio hilo inadaiwa kuwa aliachwa na wenzake ndani siku ya Sikukuu ya Idd huku mlango ukiwa umefungwa jambo ambalo lilimfanya atafute mbinu nyingine ya kutoka ndani ndipo akaamua kujirusha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Gilles Muroto amekiri kutokea kwa tukio hilo ingawa taarifa hizo zipo kwenye mitandao na hazijafikishwa kituoni hapo lakini tayari wameanza kufuatilia ili kubaini nini chanzo cha cha tukio hilo.
Hata hivyo Jina na umri wa mtoto huyo bado havijafahamika.
==>Tazama video zaidi ya tukio hilo.

Leave a Comment