×

Tiba 7 Zinazosaidia Kutotapika

LEO nitaongelea tiba ya mtu anayetapika, huenda umekula kitu kibaya kimechafua tumbo, au umekula chakula chenye sumu au ni mama mjamzito anayesumbuliwa na kichefuchefu, tumia tiba hizi.

  1. Mzizi wa tangawizi:

Mzizi wa tangawizi ni tiba nzuri kwenye suala zima la mmeng’enyo wa chakula kama una tatizo la kutapika chukua maji chemsha weka mzizi wa tangawizi kunywa taratibu, au kama tangawizi huiwezi changanya na asali, itakusaidia kwa kiasi kikubwa.

  1. Majani ya Nanaa

Kama unayo majani yaliyotengenezwa kwa Nanaa itakuwa ni vizuri sana kunywa chai yake au kama huna nenda sokoni kanunue majani yake halisi kutoka shamba yachemshe kisha kunywa kidogo kidogo yatakusaidia.

  1. Siki ya Tufaha

Ukiwa unatapika sana tumia siki ya tufaha weka kwenye maji kisha sukutua mdomoni kila unapotapika itakusaidia kuondoa kichefuchefu kinachokupata.

  1. Mdalasini

Mdalasini ni tiba nzuri sana ya kuzuia kutapika pamoja na kizunguzungu, hii ni nzuri kwa wanawake wajawazito kwa hatua zile za mwanzo ambazo wengi wao hukutwa na hali hiyo.

Tengeneza chai ya mdalasini kisha kunywa taratibu kutwa mara tatu, unaweza kuchanganya na asali.

  1. Maji ya wali:

Maji ya wali pia ni tiba nzuri sana kwenye suala zima la kuzuia kutapika, yachuje wakati unapika wali kabla hayajakauka kunywa taratibu utaona jinsi utakavyoondoa tatizo moja kwa moja.

  1. Juisi ya kitunguu maji

Juisi ya kitunguu maji ni nzuri sana kama wewe unasumbuliwa na tatizo la kutapika pia inasaidia kuondoa kizunguzungu kwa mgonjwa.

Jinsi ya kunywa juisi hiyo kama tiba kunywa kijiko kimoja kutwa mara tatu.

  1. Karafuu

Karafuu zinatakiwa kuwa kiungo kizuri kinachoweza kukupa nafuu ya haraka kwani kinasaidia mmeng’enyo tumboni lakini kwenye suala la kutapika chukua karafuu tafuna, unaweza kuchanganya na asali.

Leave a Comment