×

Dawa ya Corona Madagascar Imebuma? Mji Mkuu ‘Lockdown’

MADAGASCAR imeuweka mji  mkuu wake, Antananarivo,  kwenye ‘lockdown’ mpya kufuatia ongezeko jipya la maambukizi ya Corona Virus ikiwa ni miezi miwili tangu masharti ya ‘lockdown’ hiyo yalipolegezwa.

Taarifa kutoka Ikulu imesema,  “Mkoa wa Analamanga, ambapo mji mkuu unapatikana, unarudishwa kwenye ‘lockdown’. Hakuna atakayeruhusiwa kuingia au kutoka kwenye mkoa huo huku waliopo wakiwekewa muda wa kutoka nje.

Taratibu za ‘lockdown’ hiyo zinasema mtu mmoja pekee kutoka katika kila kaya ndiyo ataruhusiwa kutoka ndani kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa sita mchana huku sababu ikiendelea kusisitizwa ni kuongezeka kwa maambukizi.

Itakumbukwa kuwa mwezi Aprili Rais Andry Rajoelina alizindua dawa  iliyotokana na mitishamba ambapo alidai ina uwezo wa kukinga na kutibu maambukizi ya COVID-19. Pia, aliidhinisha mmea  wa ‘Artemisia’ uliotumika kutengenezea dawa hiyo kuuzwa nje ya kisiwa hicho.

Nchi kadhaa za Afrika ikiwemo Tanzania zilienda Madagascar au kuagiza dawa hiyo inayotokana na #Artemisia ambao ni mmea unaoaminika katika kutengeneza dawa za kutibu malaria.

Leave a Comment