×

Cloud 112 Aibuka na Mke Mpya Global Kutambulisha Muvi Ya ‘Usijisahau’

Staa wa filamu nchini, Issa Musa ‘Cloud 112’ akiwa na mke wake wa sasa, Mina Baby,  anayeishi nchini Sweden wakiwa Global TV Online leo kutambulisha filamu yake ya ‘Usijisahau’ itakayotoka mwezi Oktoba mwaka huu.  Filamu hiyo imetayarishiwa nchini Sweden.
Mkewe Mina Baby akimwangalia mumewe wakati akimtambulisha kabla ya kuanza mahojiano na Global TV Online.
Cloud 112 akielezea filamu yake.
Wakiwa katika pozi na mtangazaji wa Global TV Online, Isri Mohammed, baada ya mahojiano.

Nyota wa filamu nchini Issa Mussa maarufu kwa jina la Cloud 112, aliyewahi kutamba na filamu zake ikiwemo Toba, Tripple L na nyingine nyingi, amerudi upya kwenye soko la filamu baada ya kimya cha muda mrefu.

Cloud amerejea kwa kishindo baada ya kurudi kutoka nchini Sweden alipokuwa amejichimbia akitengeneza filamu yake inayoitwa Usijisahau, aliyowashirikisha wasanii Wastara Juma, Seleman Barafu pamoja na wasanii wengine wa nchini Sweden.

Prodyuza wa filamu hiyo ambaye pia ni mke mpya wa Cloud, Amina Mussa maarufu kwa jina la Mina Baby, amesema ujio mpya wa Filamu ya Usijisahau chini ya kampuni yao ya Aismu Entertainment, iliyoongozwa na Fabian kutoka Sweden, umekuja kukata kiu ya wapenzi wa filamu, kwani kumekuwa na uhaba wa muvi nzuri sokoni.

Aidha, Cloud amesema kuwa filamu hiyo itapatikana rasmi madukani kuanzia mwezi wa nane au wa tisa, hivyo anawaomba mashabiki wake na wadau wa filamu nchini kujiandaa kuipokea muvi hiyo iliyobeba utamu wa aina yake.

(Habari/ Picha: Isri Mohammed na Musa Mateja/GPL))

Leave a Comment