×

VIDEO: Manji Asomewa Mashtaka 7 Kitandani Akitibiwa Muhimbili

Yusuf Manji

Wimbi la vigogo wa ngazi na hadhi mbalimbali kufikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali na kunyimwa dhamana limeendelea baada ya leo Julai 5, 2017, mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji kusomewa shtaka la uhujumu uchumi na kunyimwa dhamana.

Washtakiwa wengine ambao wapo kwenye kesi moja na Manji wakiwa kwenye karandinga la polisi.

Waendesha mashitaka wa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu jijini Dar es Salaam, walihamia katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako Manji amelazwa na kusomewa mashtaka saba, ambayo ni kukutwa na bidhaa visivyo halali, ambavyo ni vitambaa vyenye thamani ya shilingi milioni 44, ambavyo ni mahususi kwa ajili ya kutengeneza sare za JWTZ.

 

Mawakili wa Serikali wakielekea Taasisi ya Moyo Muhimbili (JKCI) kumsomea mashtaka Yusuf Manji ambaye amelazwa.

Watuhumiwa hao wamekutwa na mihuri miwili ya JWTZ, wa kwanza ni wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, Muhuri wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na mhuri mwingine wa Commanding Officer Korogwe, plate number 2 za magari ya serikali yanayowakabili washtakiwa wanne akiwemo Manji.

Pia washtakiwa wamekutwa na shtaka la kukutwa na mihuri ya Jeshi la Wananchi Kambi ya Makutupora, Dodoma Kambi namba 834 jambo ambalo nalo ni kinyume cha sheria.

Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mtu mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja na watuhumiwa wote wamenyimwa dhamana.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 19 mwaka huu ambapo itasomwa tena huku Manji akiendelea kutibiwa Muhimbili chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi.

Pichaz na Hillali Daudi | Global TV Online

===

TAZAMA VIDEO YA TUKIO ZIMA

Leave a Comment