×

Ajibu awatia mzuka Moro

 

BAADA ya kumtambulisha rasmi mchezaji wake mpya, Ibrahim Ajibu kutoka Simba, mashabiki wa Yanga mkoani hapa, wamesema wana imani kubwa na mshambuliaji huyo na wanaamini atakuwa msaada mkubwa kwa timu yao msimu ujao.

 

Wakizungumza na Championi Ijumaa, baadhi ya mashabiki hao walisema Ajibu ni aina ya mshambuliaji mpambanaji mwenye kujituma na uwezo wa kupachika mabao, hivyo wamedai hawana wasiwasi naye.

 

Walisema kinachotakiwa kufanywa na wadau wa Yanga, ni kumsapoti huku pia wakimtaka mshambuliaji huyo kuendelea kujituma kwa mafanikio ya klabu hiyo.

 

“Ajibu ni mzuri, ni mchezaji mwenye kujituma na maarifa mengi uwanjani, naamini atatusaidia sana msimu ujao, kwake tumelamba dume,” alisema Salum Kulamali, mmoja wa mashabiki wa Yanga mkoani hapa.

Daudi Julian | CHAMPIONI

Leave a Comment