×

Tayari Nahodha wa Zamani wa Everton Ametua Dar

Leon Osman akizungumza na wanahabari baada ya kuwasili Dar

 

Mchezaji wa zamani wa Everton, Leon Osman ametua nchini leo na ataendesha mafunzo ya siku moja kwa waandishi na wachambuzi wa soka Julai 12 kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

 

 

Leon Osman akikabidhiwa kinyago kama ishara ya utalii wa Tanzania, anayekabidhi ni Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania, Godfrey Meena.

 

Ujio wa Osman ni kufungua mlango kwa Everton itakayotua nchini wiki ijayo tayari kwa mechi dhidi ya Gor Mahia ya Kenya Alhamis ijayo katika fainali ya Sportpesa utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

 

Wanahabari wakifuatilia tukio hilo.

 

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa kampuni ya Sportpesa, Abbas Tarimba  alisema msafara wa wachezaji wa Everton utatua nchini  Julai 12  na mchezaji huyo wa zamani ametangulia ili kufanya ziara ya kitalii hapa nchini.

 

Leon Osman akifunguka ujio wake nchini Tanzania.

 

“Mchezaji huyu wa zamani wa Everton ametangulia kwa  mambo makuu mawili, ambayo ni kufanya ziara ya kitalii nchini  atatembela mbuga za wanyama ya Ngorongoro siku ya Jumatatu ili kujionea vivutio mbalimbali vya kitalii vilivyopo nchini pia ataendesha semina kwa waandishi na wachambuzi wa soka

 

MJkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa kwa Upande wa Tanzania, Tarimaba Abbas Tarimba akizungumza na wanahabari.

 

Osman alisema hii ni mara ya pili kuja Tanzania na amefurahi  kuwa atapata nafasi ya kutembelea vivutio vya utalii.

Leave a Comment