×

Video: Profesa Jay Akifunga Ndoa Kanisa la St Peters, Dar

Ndoa ya Profesa Jay na mpenzi wake wa muda mrefu anayefahamika kwa jina la Grace Mgonjo, ilifungwa mchana wa Jumamosi, JULAI 08, 2017, katika Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar.

Kabla ya ndoa hiyo iliyoibua shangwe kwa ndugu, jamaa na marafiki waliofurika kanisani hapo, msafara wa kuelekea kanisani ulianzia nyumbani kwa Profesa Jay, Kimara-Temboni jijini Dar.

Ndoa hiyo ilifuatiwa na sherehe ya kukata na shoka iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar ambapo waalikwa walipata nafasi ya kula, kunywa hadi kusaza huku shughuli nzima ikipambwa na mahudhurio ya mastaa kibao wa Bongo.

Leave a Comment