×

Koeman: Hali ya Hewa Ilizingua Kidogo

Kikosi cha timu ya Everton kilichotua Tanzania.

 

KOCHA wa Everton, Ronald Koeman amesema timu yake haikuwa katika kasi ya kawaida katika kipindi cha kwanza katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, juzi Alhamisi kutoka na hali ya hewa licha ya kushinda mabao 2-1. Katika mchezo huo uliochezwa kwenya Uwanja wa Taifa jijini Dar es

Salaam, mabao ya Everton yalifungwa na Wayne Rooney dakika ya 35 na Kieran Dowell aliyefunga dakika ya 45 huku bao la Gor Mahia likifungwa dakika ya 37 na Jacques Tuyisenge.

Mchezo ukiendelea wa Everton dhidi ya Gor Mahia.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo, Koeman, 54, alisema walianza mchezo taratibu kutokana na hali ya hewa kuwa ya joto na nzito, lakini baadaye kipindi cha pili walifanya vizuri. Mchezo huo ulianza saa 11:00 jioni

na kumalizika saa 12:50, muda ambao hali ya joto huwa imepungua. “Kipindi cha kwanza hatukuwa na kazi, kwanza hii ni mechi yetu ya kujianda na msimu halafu hali ya hewa kidogo ilikuwa tatizo lakini kipindi cha pili tukacheza vizuri kwani mambo yalikuwa sawa.

Everton wakipasha walipokuwa Tanzania.

“Ni mechi nzuri kwetu hata wapinzani wetu walicheza vizuri ndiyo maana walipata bao lile, tunaondoka Tanzania na kwenda kujiandaa zaidi na msimu ujao,” alisema Koeman raia wa Uholanzi. Koeman alisema anaamini ujio wa Rooney, Davy Klaassen na Michael Keane kikosini mwake utakuwa na faida ya kufanya vizuri msimu ujao. Everton iliyoletwa Tanzania na wadhamini wao Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya SportPesa inayoidhamini pia Gor Mahia, iliondoka juzi usiku kurudi England.

Leave a Comment