×

Mwili wa Mke wa Mwakyembe Ulivyosafirishwa Baada ya Kuagwa

Jeneza likitolewa nje ya kanisa ili kusafirishwa kwenda Mbeya.

 

Gari lililobeba mwili wa marehemu.

 

Mwakyembe (katikati) akiongozana na viongozi wenzake kuelekea eneo ambapo mwili ulikuwa ukipakiwa kwenye gari kuelekea Uwanja wa Ndege kwa ajili ya kusafirishwa.

 

Jeneza likitolewa nje ya kanisa ili kusafirishwa kwenda Mbeya.

 

R.I.P Linah George Mwakyembe.

 

Jeneza likitolewa nje ya kanisa ili kusafirishwa kwenda Mbeya.

 

Jeneza likitolewa nje ya kanisa ili kusafirishwa kwenda Mbeya.

 

Ndugu wakisubili mwili wa marehemu nje ya kanisa.

 

Kanisa la KKKT lililopo Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam ambapo mke wa Mwakyembe aliagwa mapema leo.

 

Jeneza lenye mwili wa marehemu likifunikwa tayari kwa safari ya kwenda Kyela Mbeya kwa Mazishi.

 

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi Samia Suluhu Hassan amewaongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa aliyekuwa mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, Bi. Linah George Mwakyembe katika Kanisa la KKKT lililopo Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.

 

Wakati wa kuaga mwili wa marehemu Linah, viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais, Katibu Mkuu balozi John Kijazi na wengine walipata fursa ya kutoa salam za pole kwa familia ya Dkt. Mwakyembe kwa kuondokewa na ndugu yao kipenzi.

 

“Tunajua Linah alikuwa zaidi ya kila kitu kwenu, lakini tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kazi yake. Alimleta dada Linah duniani, alitupa amana yake na leo ameinyakua. Sisi tulimpenda lakini Mwenyezi Mungu amempenda zaidi. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe!” alisema Samia.

Leave a Comment