×

NMB Yaja na ‘Trade Finance’ Kuendeleza Uchumi wa Viwanda

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker akizungumza katika warsha iliyoandaliwa na benki hiyo kuhusu huduma ya Trade Finance. Pembeni yake ni Mkuu wa Kitengo cha Trade Finance,Linda Mtango.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

BENKI ya NMB imekuja na huduma ijulikanayo kama ‘Trade Finance’ yenye lengo la kuendana na mabadiliko na kuendeleza uchumi wa viwanda nchini.

Trade Finance ni utaratibu wa benki ambao unamwezesha mteja kama Mkandarasi, Wazalishaji na Wasambazaji kupata bidhaa na huduma za kibiashara ndani na nje ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker, amesema kuwa huduma hiyo inahusika na manunuzi na kuleta vifaa mbalimbali kutoka nje ya nchi na usafirishaji wa vifaa na bidhaa mbalimbali.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Trade Finance, Bi. Linda Mtango , amesema kitengo hicho kinahusika pia katika udhamini kwa mteja endapo atashindwa kulipia huduma hiyo.

Pia amesema kuwa benki italazimika kufanya mapitio ya taarifa za mteja pale inapotokea mteja huyo kuhitaji dhamana.

Leave a Comment