
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Msajili wa Vyama, Prof. Ibrahim Lipumba, akanusha ripoti kwamba chama hicho kimeitisha Mkutano wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa utakaofanyika huko Zanzibar kesho Ijumaa, Agosti 28, kama ilivyosambazwa kwa njia ya ujumbe wa simu na Donald Bashange akiwa Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF.
Lipumba alisema kuwa akiwa mwenyekiti wa chama hicho na Kaimu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya, hawana habari na mkutano huo.