×

RONALDO MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUKWEPA KODI

ronaldo mahakamani kwa tuhuma za kukwepa kodi
Endapo atakutwa na hatia, atafungwa miaka mitatu na nusu

Mwanasoka Cristiano Ronaldo leo amefika mahakamani huko Hispania kwa tuhuma ya kukwepa kodi.

Mwanasoka huyu anatuhumiwa kwa kukwepa kiasi cha €14.7m ($17.3m; £13.1m) tangu mwaka  2010 ambazo ni sawa na Tsh. Bilioni 38.

Hata hivyo, nyota huyo wa Real Madrid amekana mashtaka hayo.

Nyota wa Argentina, Lionel Messi, anayechezea Barcelona, alihukumiwa kifungo cha miezi 21 jela baada ya kukutwa na hatia kama anayotuhumiwa Ronaldo.

1 Comment

Leave a Comment