×

Watoto Mapacha Waliozaliwa Wameungana Morogoro Kutenganishwa

Dk. Zaituni Bokhari.

Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Zaituni Bokhary amesema baada ya kufanya vipimo, imegundulika kuna uwezekano wa kuwatenganisha watoto mapacha waliozaliwa wakiwa wameungana mkoani Morogoro.

Dk Bokhary ambaye amebobea katika upasuaji huo Afrika Mashariki,  ameyasema hayo leo asubuhi alipokuwa akitoa majibu ya vipimo vilivyochukuliwa hospitalini hapo kwa takribani wiki nzima.

 

Watoto walioungana.

 

“Vipimo vya damu vimeonyesha kila mtoto ana mfumo wake na hawana maambukizi ya aina yoyote, ugumu unakuja kwenye ini na moyo ambapo wanategemeana ila uwezekano wa kutenganishwa upo,” amesema Dk Bokhary.

 

Wazazi wa watoto hao.

 

Majibu hayo yamekuja siku chache baada ya pacha hao kupimwa vipimo vya radiolojia ikiwemo CT Scan, MRI, X Ray kipimo cha moyo (ECO) pamoja na vipimo vyote vya damu.

 

Mkunga akiwa amewabeba watoto hao.

Watoto hao waliozaliwa katika hospitali ya Misheni ya Berega iliyopo Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro, Julai 21 mwaka huu wamenaza kuchukuliwa vipimo mbalimbali vya awali.

VIDEO: Baba wa Watoto Waliozaliwa Wameungana Aomba Msaada

 

 
 

Leave a Comment