
RAIS John Magufuli amefuta hati ya mashamba matano yenye zaidi ya ekari 14,000 zilizochukuliwa na watu na wakashindwa kuyaendeleza, wilayani Muheza mkoani Tanga.
Hayo ameyasema leo huko Mkanyageni wilayani humo wakati akianza ziara yake ya siku tano mkoani Tanga na kuongeza kuwa mashamba hayo ameyakabidhi kwa uongozii wa mkoa ili waweke utaratibu maalum wa kuyagawa huku akiagiza sehemu kubwa ya mashamba hayo wapewe wananchi bure.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella amesema mashamba hayo yaliyofutwa hati zake wamepanga kila mwananchi apewe heka tatu kwa ajili ya kilimo.