
Hali ya dharura imetangazwa nchini Sudani katika majimbo sita kutokana na mafuriko yaliyo haribu makazi na kusababisha vifo vya watu 100.
Ofisi ya umoja wa mataifa inayoratibu maswala ya kibinadamu imesema zaidi ya watu laki mbili wameathiliwa na mafuriko hayo katika majimbo 15 kati ya majimbo 18.

Mvua za vipindi nchini sudan mwaka jana zilisababisha vifo vya watu 80 na kuharibu makazi ya watu tofauti ikiwemo na kufunika nyumba za watu mbalimbali na kupoteza makazi ya watu wa nchi hiyo.
Pia katika mwaka 2020 takribani watu laki nane waliathiliwa na mafuliko yalio tokea na kupelekea hali ya dhalura kutangazwa nchini sudani.
Imeandikwa: leocardia Charles kwa msaada wa mitandao.