×

Omog: Namtafutia Niyonzima Kamusoko Mpya

Kiungo mpya wa Yanga, Haruna Niyonzima.

KOCHA Mkuu wa Simba, Joseph Omog raia wa Cameroon, amesema kiungo wake mpya, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda, atapewa mtu maalum wa kucheza naye kwenye kikosi hicho ili kuendelea kuonyesha makali yake kama aliyokuwa akiyaonyesha ndani ya Yanga.

Niyonzima ambaye amejiunga na Simba hivi karibuni akitokea Yanga na kupewa mkataba wa miaka miwili, anaimudu vema nafasi ya kiungo wa kati ambapo wakati yupo Yanga, alikuwa akishirikiana vizuri sana na Thaban Kamusoko na kuonekana ni fundi zaidi.

 

Omog ameliambia Championi Jumatano, kuwa, kutokana na uzuri na ufundi aliokuwa nao Niyonzima, ni wazi anatakiwa kuchezeshwa na wachezaji wazuri ili asiwe na kazi kubwa uwanjani ya kufanya zaidi ya kutimiza majukumu yake.

 

“Niyonzima ni mchezaji mzuri ambaye atatusaidia sana kwenye kikosi chetu, ujio wake hauwezi kubadili mfumo tutakaoutumia, lakini tutakachokifanya ni kumpa nafasi acheze na watu maalum ambao wataendana uchezaji wao ili kumpunguzia kazi awapo uwanjani.

 

“Unajua kikosi chetu cha hivi sasa ni cha tofauti sana, ukiangalia kina wachezaji wengi wenye uwezo wa hali ya juu ambao ukiwapa nafasi hawawezi kukuangusha hata kidogo, hivyo itakuwa kazi kwetu kuona siku fulani nani anafaa kucheza na nani, na yupi acheze siku nyingine ili awe huru kama alivyokuwa anacheza na Kamusoko pale Yanga,” alisema Omog.

Esha Buheti: Jini Kabula Kweli Anaumwa, Tumsaidieni!

Leave a Comment