×

William Ngeleja: Seduce Me ya Alikiba Sio Level ya Bongo -(VIDEO)

Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (CCM) ameshindwa kujizuia na kufunguka kuhusu alivyoguswa na wimbo mpya wa Alikiba, ‘Seduce Me’ huku akimmwagia misifa msanii huyo kuwa wimbo aliuachia ni wa kiwango cha juu.

“Ukiacha siasa mimi ni mdau mkubwa wa sanaa na michezo, napenda sana muziki, wimbo mpya wa Alikiba ‘Seduce Me’ umenigusa sana, ni wimbo mzuri wenye mahadhi ya taaluma ya muziki.

“Huu wimbo si wa level ya Tanzania, unatakiwa kuwa wimbo wa Kimataifa kwa kuwa unaweza kupigwa Japan, Marekani, China na nchi nyingine kubwa nje,” alisema Ngeleja.

Leave a Comment