×

LIVE: Aliyeibiwa Mtoto wa Miaka 2 Ampata Akiwa na Miaka 15, DNA Utata


MAMA Shamim Juma mkazi wa Dar es Salaam ambaye ni mwenyeji wa mkoani Mwanza anadai kuwa aliibiwa mwanaye wa miaka miwili, kisha kumpata akiwa mkubwa wa umri wa miaka 15.

Baada kufuatilia inadaiwa kuwa mtoto huyo aliibwa na bibi mmoja ambaye alikuwa mfanyakazi wao wa ndani. Baada ya ndugu wa Shamim kubaini mtoto wa ndugu yao alipo walimpa taarifa mhusika na kuripoti katika kituo cha polisi ambapo bibi huyo alikamatwa ili aeleze alimpata wapi mtoto huyo.

Shamim Juma.

Shamim anasimulia kuwa yule bibi alikana kumuiba mtoto huyo na kusema kuwa ni mjukuu wake (mtoto wa binti yake)  hivyo taratibu za kisheria zilifuatwa hadi kesi ikafika kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kupima DNA (Vinasaba) kubaini mzazi halali wa mtoto huyo.

Anadai majibu ya DNA ya Mkemia hayakuonyesha vizuri kwa mara ya kwanza hivyo waliambiwa wapime tena kwa mara nyingine….. bibi ameshaachiwa na polisi…. mtoto yuko wapi?….

Nisikumalizie uhondo… fuatilia mkasa huo kupitia Global TV Online.

Subscribe sasa ===> Global TV Online.

Leave a Comment