×

R.O.M.A ni Freemason?

R.O.M.A Mkatoliki.

R.O.M.A ambaye jina halisi alilopewa na wazazi wake ni Ibrahimu Mussa, si jina geni kwenye ulimwengu wa burudani, ni jina la mwanamuziki wa Hip Hop mwenye mashabiki wengi kila kona ndani na nje ya Bongo.

Ukiachana na hilo, R.O.M.A ni mwanamuziki mbunifu. Ukitazama video za nyimbo zake pamoja na matamasha yake kwenye Mtandao wa Global TV Online na YouTube utakubali juu ya suala hili.

Alama za Freemason.

Hata hivyo kinachovuta hisia za watu wengi katika ubunifu wake ni namna ambavyo amekuwa mara kwa mara akijifananisha na kiongozi wa ibada katika imani f’lan jambo ambalo limefanya kuwepo na maswali juu yake na kumuhusisha na watu wanaoamini kupitia taasisi ya wajenzi huru, Freemason.

Suala la wasanii duniani kote kuhusishwa na taasisi hiyo si geni! Wapo wanamuziki na waigizaji wengi wamehusishwa kuwa Freemason na hiyo ni kutokana na namna wanavyofanya ubunifu katika kazi zao.

Kanumba.

Mfano hawa hapa;

Hapa Bongo muigizaji nguli, marehemu Steven Kanumba aliwahi kuhusishwa kuwa Freemason kutokana na ubunifu katika mavazi yake pamoja na kazi zake ikiwemo Devil’s Kingdom.

Mbali na Kanumba, mwanamuziki Nay wa Mitego pia amewahi kuhusishwa kuwa Freemason hasa kutokana na mali alizonazo lakini kubwa hasa ni sanamu ambalo limepamba sebuleni kwake. Ni sanamu jeusi la mtu aliyepiga magoti na kuficha kichwa katikati ya mapaja na kunyo-osha mikono pembeni.

ROMA Dar Live.

Juu ya sanamu hilo Nay amekuwa akisema lina siri kubwa bila kutaja ni siri gani. Lakini pia nembo ya lebo yake ya Freenation ambayo ni mabawa yaliyochanua nayo huwa inahusishwa na mambo a Kifreemason.

Sasa vipi kuhusu R.O.M.A naye ni Freemason? Hilo ndilo swali la msingi kwa sasa.

Jay-Z.

Anaungana na hawa

R.O.M.A kwa mbele unaweza kumfananisha au kumuunganisha kwenye kundi moja na kina Jay-Z, Kanye West, Taylor Swift na hata Lady Gagga kwenye upande wa ubunifu katika kazi zao. Kila mmoja wao kuna ‘image’ f’lan ambayo amejijengea kwa mashabiki wake kwenye suala zima la ubunifu.

Huku R.O.M.A akitoka mara kwa mara kama kiongozi wa dini, Taylor Swift amekuwa akiibuka na video zinazoonesha mambo ya ajabu ambayo si rahisi kutokea kwenye ulimwengu.

BONIPHACE NGUMIJE | IJUMAA.

Breaking News: Polisi, TCRA Watoa Kauli Kuhusu Usambazaji Taarifa Mitandaoni

Leave a Comment