
SOKA la sasa ni biashara, klabu nyingi zimekuwa zikipata nguvu kubwa kutokana na udhamini, hivyo ndivyo inavyoonekana kwa Klabu ya Majimaji ambayo ni moja ya klabu kongwe nchini, baada ya kupata udhamini wa mwaka mmoja wa Kampuni ya Sokabet.
Kampuni hiyo inayojihusisha na michezo ya kubashiri matokeo, imeonyesha dalili za kuipa nguvu Majimaji ambapo tayari mwitikio wake ndani na nje ya klabu hiyo ni mkubwa.
Kabla ya udhamini huo, Majimaji ilikuwa ikionekana kutokuwa vizuri kiuchumi, kuthibitisha hilo ni jinsi ilivyo safari ya usiku mnene kutoka Songea kuelekea Mbeya kwa basi na kuingia Mbeya asubuhi ya siku ya mchezo wao dhidi ya Mbeya City, hivi karibuni.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara, Majimaji ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0, lakini kabla ya kucheza mchezo uliofuata dhidi
ya Prisons, Majimaji ilipata bahati ya kusaini mkataba na Sokabet wenye thamani ya Sh milioni 150.
Kwenye mchezo dhidi ya Prisons, Majimaji iliwasili Mbeya mapema na ilifanikiwa kutoka sare ya bao 2-2 huku wachezaji wake wakicheza vizuri kwa asilimia kubwa. Mchezo unaofuata wikiendi hii itakumbana na Yanga katika kipute kitakachopigwa kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea.
Leo Jumamosi, Majimaji itaivaa Yanga na inaelezwa kuwa wapo fiti na tayari kwa ajili ya mchezo huo wa Ligi Kuu Bara, je, unafahamu ni kwa namna gani Sokabet wamepokewa Songea? Ifuatayo ni mitazamo ya Wanalizombe hao:

OFISA HABARI WA MAJIMAJI
“Wazungu wanasema something is better than nothing, kwa maana ya bora kupata kidogo kuliko kukosa kabisa, sisi tumewapokea Sokabet kwa furaha kubwa mno, na tutafanya nao kazi vizuri kwa manufaa yetu sote.
“Sokabet wametuokoa kwenye kipengele cha mishahara, viongozi tunajipanga ili kuhakikisha tunaweka mazingira rafiki ya kufikisha jezi zenye nembo ya Sokabet kwa mashabiki wetu,” anafafanua Ofisa Habari wa Majimaji, Onesmo Ndunguru.
MENEJA WA MAJIMAJI
“Wachezaji wetu baada ya kusikia tumepata ufadhili huu wamezidisha juhudi za kupambana uwanjani, tunakutana na Yanga kikosi chetu kikiwa vizuri kisaikolojia na kifiziki naamini tutaibuka na ushindi.
“Pia tunaomba msimu ujao wasituache kwa kuwa udhamini wao ni muhimu sana kwetu,” anafafanua Godfrey Mvula ambaye mwaka huu ametimiza miaka 17 ya umeneja ndani ya timu hiyo.
KOCHA WA TIMU
“Ni udhamini mzuri, tunashukuru wametuunga mkono. Viongozi waendelee kutafuta wadhamini wengine ili tunufaike zaidi,” anasema Peter Mhina, kaimu kocha mkuu.
Sokabet… Shinda Milioni 100
WACHEZAJI
“Sisi kwa upande wetu tume furahia sana na kama inavyofahamika mpira wa siku hizi ni fedha. Majimaji mara nyingi inafanya vibaya kwa kukosa fedha. Udhamini wao utatusaidia sana,” anasema Danny Mrwanda ambaye ni nahodha wa timu hiyo.
Akizungumzia juu ya udhamini huo, Mratibu wa Sokabet, Franco Ruhinda anasema mipango ya kampuni yao ni kukuza mchezo wa soka na mingine, kwa kuanzia wameanza na Majimaji lakini baada ya hapo mipango yao ni mikubwa katika jamii ya Tanzania, ambapo udhamini huo ni kurejesha kwenye jamii kile ambacho w a t a k u w a w a k i k i p a ta katika michezo ya kubashi r i matokeo.
A i d h a , F r a n c o a l i o n g e z a kuwa wale wanaotaka kubashiri matokeo wanaweza kufanya hivyo kwa kufungua tovuti ya www.sokabet.co.tz ambapo kwa kutumia namba ya kampuni ya 335757 wanaweza kuingiza fedha kwenye akaunti zao na kubet.
Anafafanua zaidi kwa kusema, baada ya kufungua akaunti mtumiaji anaweza kuingiza fedha kisha kuanza kubeti.
Anasema kwa watumiaji wa Vod a com wanaweza kuingiza salio kwa kubonyeza *150*00#, chagua namba 4 (lipa kwa M-pesa), chagua namba 4 (weka namba ya kampuni), ingiza namba ya kampuni ambayo ni 335757, kisha ingiza kumbukumbu ambayo ni neno ‘Sokabet’.
Baada ya hapo ingiza kiasi unachotaka mfano Sh 1,000 au 5,000 na kuendelea, utamalizia kwa kuingiza namba yako ya siri na bonyeza namba 1 kukamilisha mchakato.
Kwa Tigopesa, bonyeza *150*01#, chagua namba 4 (lipia bili), bonyeza namba 3 (ingiza namba ya kampuni), ingiza namba 335757, kisha ingiza kiasi cha fedha, ingiza neno ‘Sokabet’, malizia na namba yako ya siri ya Tigopesa.
Kwa Airtel bonyeza *150*60#, chagua namba 5 (lipia bili), bonyeza namba 4 (namba ya kampuni), ingiza namba 335757, kisha ingiza kiasi cha fedha, itakwambia ingiza kumbukumbu namba (hapa ingiza neno ‘Sokabet’), kisha namba yako ya siri ya Airtel money.
MAKALA, CHAMPIONI JUMAMOSI