
MSANII wa filamu za Kibongo, Koletha Raymond anadaiwa kupigwa stop kucheza filamu na mumewe Temba ndiyo maana amejikita kwenye mambo mengine kwa sasa.
Chanzo kilieleza kwamba kutokana na tabia za baadhi ya wasanii wa kike kutojiheshimu hata kama wakiwa kwenye ndoa, mume wa Koletha ameamua kumpiga stop kucheza filamu ili kulinda ndoa yao isije kukumbwa na kimbunga kwani ndoa nyingi za mastaa zimekuwa hazidumu.
Usipitwe na Matukio, Install App Yetu ya Global Publishers
Android ===>Google Play
iOS ===>Play Store
Alipoulizwa Koletha kuhusiana na madai hayo alikuwa na haya ya kusema; “Kiukweli mume wangu hajawahi kunikataza kucheza filamu na hawezi kuniachisha kazi hii maana alinikuta ninaifanya labda atanipa mipaka tu ya kucheza, nimepumzika tu kwa muda nafanya mambo mengine.”