×

Obrey Chirwa, Ajibu Watengenezwa Upya Yanga

Kikosi cha timu ya Yanga.

 

KATIKA kuhakikisha anaimarisha safu yake ya ushambuliaji, Kocha Mkuu wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina ameanza kuwasuka upya washambuliaji, Ibrahim Ajibu na Obrey Chirwa.

 

Hiyo imetokea siku chache wakiwa wametoka kushinda mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar katika Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba. Mabao ya Yanga yalifungwa na Ajibu na Chirwa.

 

Mzambia huyo, amefikia hatua hiyo ya kuwasuka nyota hao baada ya Donald Ngoma kutopona haraka majeraha ya nyama za paja na huenda akawa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Wachezaji wa timu ya Yanga wakipongezana.

Mmoja wa watu wa benchi la ufundi la Yanga, ameliambia Championi Jumamosi kuwa, Lwandamina ameanza kutengeneza kombinesheni itakayoelewana na kucheza muda mrefu ya Ajibu na Chirwa wakati Ngoma akiwa anauguza majeraha yake.

 

Mtoa taarifa huyo alisema, kocha huyo amemhamisha Chirwa kucheza namba tisa nafasi iliyokuwa inachezwa na Ngoma. Zamani Chirwa alikuwa akicheza pembeni.

 

“Benchi la ufundi limefurahishwa na uchezaji mzuri wa ushirikiano wao kwa maana ya kombinesheni iliyocheza kwa kuelewana kwa muda mfupi na kufanikiwa kupata ushindi katika mechi iliyopita na Kagera.

 

“Kama unavyojua tangu ligi imeanza Ajibu na Chirwa hawakuwahi kucheza pamoja namba tisa na kumi, lakini mechi dhidi ya Kagera walicheza kwa mara ya kwanza na wakafanya vizuri na kila mmoja akafunga,” kilisema chanzo chetu.

 

Alipotafutwa Lwandamina alisema: “Nataka kila mchezaji awe na uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja na hiyo ndiyo falsafa yangu, ninafurahia kuona ushirikiano mzuri wa Ajibu na Chirwa.

Stori: Wilbert Molandi | Championi Jumamosi

Yanga Yadaiwa Kuipokea Njombe Mji ,Wailipia Hotel Kuihujumu Simba

Leave a Comment