
WAKATI kikosi cha Yanga kikiwa katika maandalizi yake makali ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba itakayochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar, mabeki wa kati wa timu hiyo, Kelvin Yondani na Andrew Vincent ‘Dante’ wamepewa mbinu za kumzuia Emmanuel Okwi ili asilete madhara langoni kwao.
Akizungumza na Championi Jumatano, beki wa kati wa Mtibwa Sugar, Dickson Daudi, alisema kuwa, Yondani na Dante wanatakiwa kuhakikisha wanacheza mipira yote ya juu lakini pia wahakikishe Okwi hapati nafasi ya kupiga shuti.
Alisema, jambo jingine ambalo wanatakiwa kuwa nalo makini katika mechi hiyo ni kuhakikisha wanacheza mipira yote ya juu ambayo itakuwa ikipigwa langoni kwao.
“Wakifanikiwa kufanya hivyo ni matumaini yangu kuwa Okwi watamdhibiti na hataleta madhara langoni kwao kama tulivyofanikiwa kumdhibiti sisi tulipokutana na Simba hivi karibuni kwenye Uwanja wa Uhuru.
“Katika mechi hiyo tulihakikisha hapati nafasi ya kupiga shuti au kukimbia na mpira lakini pia mipira yote ya juu tulikuwa tunaicheza sisi, ndiyo maana hakuleta madhara kabisa langoni kwetu,” alisema Daudi.
Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers
Android Bofya ===> Google Play
iOS Bofya ===>Apple Store
Stori: Sweetbert Lukonge | Global Publishers