
USIKU wa kuamkia leo, Shindano linalodhaminiwa na kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia StarTimes na chaneli yake ya Star Swahili lilifikia mwisho huku washindi 10 wakiibuka kidedea katika mchakatio wa kuwasaka machampioni hao

Miongoni mwa watu walioibuka washindi ni Msanii wa filamu Bongo, Koletha Raymond, aliyeibuka mshindi namba moja baada ya kuwabwaga washiriki zaidi ya 25, aliyokuwa akichuana nao kwa ajili ya kuwania nafasi ya kwenda kufanya kazi makao makuu ya Kampuni ya Star Times, nchini China kuigiza sauti ya filamu mbalimbali zilizochezwa kwa lugha mbalimbali.

Shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa LAPF lililopo Millenium Tower Kijitonyama jijini Dar es Salaam, ambapo washindi 10, wataungana na Koleta kwenda nchini humo kwa ajili ya kufanya kazi hiyo ambayo wataifanya kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Washindi hao wamepatikana katika ushindani mkali mbele ya majaji watatu wakiongozwa na wasanii Jacob Steven ‘JB’ na Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ ambapo haikuwa kazi rahisi kwa majaji hao na washiriki wenyewe kutokana na ushindani mkali uliojitokeza.


Mmoja wa waigizaji maarufu nchini, Muhogo Mchungu alijikuta akiangukia pua baada ya kuzidiwa ujuzi na vijana.





