×

Polisi Wachukua Simu Ya Zitto Kabwe

Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe (katikati).

Kiongozi wa Chama cha ACT – Wazalendo ameripoti katika Kituo cha Uchunguzi wa Makosa ya Kiuchumi, Kamata, Kariakoo kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu takwimu za pato la taifa alizozitoa hivi karibuni.

 

Baada ya kuwasili kituoni hapo, Jeshi la Polisi limechukua simu ya Mh. Zitto na kuishikilia kwa maelezo kuwa itasaidia uchunguzi wao.

 

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma, Ado Shaibu amesema kuwa baada ya kuichukua simu hiyo, wameahidi watairudisha kwake jioni ya kesho huku akitakiwa kuripoti kituoni hapo Novemba 27, mwaka huu.

 

Pia ameeleza kuwa Jeshi la Polisi limetoa taarifa kuwa litakwenda katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha ACT – Wazalendo, kwa Lengo la kufanya upekuzi wa ofisi hizo kutafuta nyaraka zilizotumika na chama kufanya uchambuzi wa takwimu za serikali ambao unaonesha uchumi wa nchi yetu unasinyaa.

 HABARI: DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

Leave a Comment