
Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel leo imezindua programu yake ya ‘Graduate Sales Force Project’ yenye lengo la kuwapa ujuzi wahitimu wa vyuo vikuuambao bado hawajapata kazi rasmi kabla ya kuingia kwenye Soko la ajira.
Akizungumzia programu hiyo katika Makao makuu ya Kampuni hiyo leo jijini Dar es salaam, Meneja Mauzo na Usambazaji wa Zantel, Haidari Chamshama alisema “Programu hii ni ya mwezi mmoja na ina lengo la kuwanufaisha wahitimu wa vyuo mbalimbali ambao bado hawana ajira rasmi kwa kufanya kazi kwenye vitengo mbalimbali katika Kampuni ya Zantel”.
Kwa sasa programu hiyo itajikita kwenye Masuala ya Mauzo na wataangalia jinsi ambavyo wahitimu hao wanavyojituma kazini na hatimae kuajiri wachache kati yao.

Kwa Upande wake Meneja wa Chapa na Mawasiliano Zantel, Rukia Mtingwa alisema Soko la ajira limekua gumu kwa hivi sasa hivyo, Zantel wameona ni vyema kuwapa ujuzi wanahitimu wa vyuo mbalimbali ili kuwajengea ujuzi kabla ya kuingia ya kujipatia ajira.
Jumla ya wahitimu ni 95 kutoka vyuo 15 vya Tanzania wa fani tofauti wamechukuliwa kwa mwezi huu na Zantel kwa ajili ya mafunzo hayo kwa vitendo.