Mzee wa ‘900 Itapendeza’ Atinga Global, Afunguka Mazito
Global Publishers November 15, 2017 0 Comments
SHARE THIS:
Mtangazaji wa Global TV, Catherine Kahabi akiwa na Dkt. Louis Shika maarufu kama ‘900 Itapendeza’ wawasili katika ofisi za Global Publishers zilizoko Sinza-Mori, jijini Dar es Salaam.Dkt. Shika (katikati) akisaini kitabu cha wageni.…Akitembezwa ndani ya ofisi ya Global Group.…Akiingia kwenye sehemu ya Magazeti Pendwa.…Akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Group, Eric Shigongo (kushoto) kuhusu mkasa uliompata wakati wa mnada wa nyumba za Lugumi.Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally (kulia) akimsikiliza kwa makini Dkt. Shika.
Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kushoto) akisalimiana na Dkt. Shika. Katikati ni Catherine Kahabi.Mhariri wa gazeti la Ijumaa Wikienda, Sifael Paul (kulia) akibadilishana maneno na Dk. Shika, Kahabi akiwa pembeni yao.Mhariri wa gazeti la Championi Jumamosi, Elius Kambili (kulia) akiteta jambo na Dk. Shika. Wengine kulia ni mhariri Lucy Mgina, Martha Mboma (wa tatu kulia).Dkt Shika akisalimiana na mwandishi wa habari Amos Crispin.…Akiwa na (toka kulia) msanifu kurasa Ayubu Dotto, mhariri Walusanga Ndaki, msanifu kurasa Asteria Aaron na Kahabi. Meneja wa Vipindi wa Global TV, James Range (kushoto) akisalimiana na Dkt. Shika.…Akiwa na Sifael Paul na Mhariri Mwandamizi wa gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli (kushoto) wakati wa mahojiano kuhusu yaliyompata.…Dkt Shika akifunguka kuhusu yaliyompata.
Dkt. Louis Shika, aliyejipatia umaarufu mkubwa baada ya kuibuka mshindi wa mnada wa nyumba tatu za kifahari za bilionea Lugumi, leo ametinga kwenye ofisi za Global Publishers, Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.
Dkt. Shika ambaye alishikiliwa na jeshi la polisi kwa siku kadhaa tangu kufanyika kwa mnada huo baada ya kushindwa kulipa malipo ya awali aliyotakiwa kulipa, amepata fursa ya kukutana na viongozi mbalimbali wa Kampuni ya Global Publishers na wafanyakazi ambapo pamoja na mambo mengine, amefanya mahojiano ‘exclusive’ yanayopatikana Global TV Online kupitia Youtube.