
FT: Yanga 5-0 Mbeya City
Dakika ya 90: Zinaongezwa dakika 3 za nyongeza.
Dakika ya 85: Mashabiki wa Yanga wanaongeza kasi ya kushangilia.
Dakika ya 85: Mashabiki wa Yanga wanaongeza kasi ya kushangilia.
Dakika ya 80: Bao la tano kwa Yanga linapatikana kupitia kwa Emmanuel Martine ambaye anamalizia kazi ya Gadiel Michael.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dakika ya 75: Chirwa anapambana kutengeneza nafasi lakini anashindwa kuwatoka walinzi wa Mbeya City.
Dakika ya 71: Juma Abdul wa Yanga yupo chini ameumia mguu.
Dakika ya 70: Mbeya City wanaonekana kupunguza kasi yao ya kujipanga.
Dakika ya 68: Mbeya City wanafanya mabadiliko, anatoka Mrisho Ngassa, anaingia Victor Hangaya.
Dakika ya 68: Yanga wanaendelea kulisakama lango la Mbeya City.
Chirwa anaipatia Yanga bao la nne akiunganisha pasi ya Ibrahim Ajibu.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dakika ya 58: Kasi inaongezeka kwa Yanga wanaonekana kuwa wametulia zaidi.
Dakika ya 50 Obrey Chirwa anatupia kambani na kuandika bao la tatu
Dakika ya 50: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dakika ya 47 Yanga wanapata penati
MAPUMZIKO
Dakika ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 4 za nyongeza, wakati huohuo, Martine wa Yanga yupo chini ameumia mguu wa kushoto.
Dakika ya 44: Ajibu anafika kwenye lango la Mbeya City lakini anakuwa ameotea.
Dakika ya 43: Buswita yupo chini ameumia, amechezewa faulo na Mwasapili ambaye amepewa kadi ya njano kwa mchezo mbaya.
Dakika ya 40: Kasi ya mchezo imepungua kiasi.
Dakika ya 34: Beki wa Yanga, Juma Abdul anapata nafasi ya kupiga sguti langoni mwa Yanga, mpira unatoka nje.
Dakika ya 32: Mbeya City wanapata faulo.
Dakika ya 30: Pius Buswita wa Yanga anabaki na kipa, miguu yake inapata kigugumizi, anashindwa kumalizia kazi nzuri aliyoifanya, mpira unaokolewa. Martine wa Yanga anapewa kadi kwa kucheza faulo.
Dakika ya 28: Mbeya City ni kama wameamka, wanajaribu kujipanga lakini mambo ni magumu.
Yanga wanafunga bao la pili kupitia kwa Emmanuel Martine, aliyewatoka walinzi wa Mbeya City na kufunga.
Dakika ya 22: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Yanga wanapata bao la kwanza kupitia kwa Obrey Chirwa, anafunga baada ya uzembe wa mlinzi wa Mbeya City.
Dakika ya 19: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dakika ya 18: Mbeya City wanakuwa wabishi kuwaruhusu Yanga kucheza soka la pasi nyingi.
Dakika ya 14: Mbeya City wanalisogela lango la Yanga lakini wanakosa umakini.
Dakika ya 12: Mchezaji mmoja wa Mbeya City yupo chini akipatiwa matibabu.
Dakika ya 14: Mbeya City wanalisogela lango la Yanga lakini wanakosa umakini.
Dakika ya 12: Mchezaji mmoja wa Mbeya City yupo chini akipatiwa matibabu.
Dakika ya 6: Mchezo haina kasi kubwa.
Dakika ya 4: Kocha wa Yanga, George Lwandamina ameshasimama.
Dakika ya 1: Mchezo umeanza ka kasi ndogo.
Mwamuzi anaaznisha mchezo.
Huu ni mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, unachezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
(LIVE UPDATES NA: NICOLAUS TRAC , GLOBAL PUBLISHERS)