×

Rais Kenyatta Kuapishwa Jumanne Wiki Ijayo

Rais Kenyatta.

Rais Kenyatta sasa anatarajiwa kuapishwa kuwa Rais kwa muhula wa pili baada ya Mahakama ya Juu kufutilia mbali kesi ambazo zilikuwa zinapinga ushindi wake katika uchaguzi wa marudio uliofanyika tarehe 26 Oktoba.

Kifungu 141(1b) cha Katiba ya Kenya kinasema Rais anafaa kuapishwa siku ya saba inayofuata siku ya kutolewa kwa uamuzi wa mahakama wa kuidhinisha uchaguzi iwapo kulikuwa na kesi iliyokuwa imewasilishwa.

Rais, kwa mujibu wa katiba, anafaa kuapishwa hadharani mbele ya Jaji Mkuu au Naibu Jaji Mkuu.

Mahakama Kenya yatupilia mbali kesi zilizopinga ushindi wa Kenyatta

Jaji Mkuu, David Maraga.

Mahakama ya Juu Kenya imetupilia mbali kesi mbili zilizokuwa zimewasilishwa kupinga uchaguzi wa marudio, na hivyo imeidhinisha ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta.

Jaji Mkuu David Maraga amesema majaji kwa kauli moja wameamua kwamba kesi zote mbili hazina msingi.  Kesi ya mbunge wa zamani Bw Harun Mwau na wanaharakati wawili Njonjo Mue na Khelef Khalif zimetupiliwa mbali.

“Uchaguzi wa 26 Oktoba umedumishwa, sawa na ushindi wa Bw Kenyatta. Kila upande utasimamia gharama yake,” amesema.

Uamuzi wa kina utatolewa katika kipindi cha siku 21.

 

Leave a Comment