×

Wanasayansi Wabaini Ziwa Victoria Huenda Likakauka

Wanasayansi wanasema kwamba Ziwa Victoria ambalo ni kubwa zaidi lenye maji tulivu Barani Afrika linalounganisha nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, lipo katika hatari kubwa ya kukauka.

Wanasema kwamba uvuvi haramu na uliopitiliza pamoja na uvamizi wa mazingira kuzunguka maeneo ya ziwa ni sababu kubwa ya kukauka kwa Ziwa hilo.

Maji machafu pia yanayotiririshwa kuelekea kwenye ziwa hilo yanahatarisha usalama wa viumbe vya majini.

Jeshi la Uganda limeweka mipango maalum ikiwa ni pamoja na kuharibu nyenzo za uvuvi haramu zinazotajwa kuwa miongoni mwa sababu.

Leave a Comment