×

MAKUNDI YOTE WORLD CUP 2018 HAYA HAPA, RONALDO APANGWA NA RAFIKI ZAKE

Upangwaji wa makundi wa michuano ya Kombe la Dunia ambayo itafanyika mwakani nchini Urusi umefanyika leo nchini humo.

Michuano hiyo ambayo ni mikubwa katika ngazi ya soka kuliko yote duniani inatarajiwa kuanza Juni 14 na kumalizika Julai 15, ambapo nchi 32 zitashiriki kutoka mabara matano.

Kutakuwa na viwanja 12 na miji 11 ambayo itatumika katika michuano hiyo.

Staa wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ambaye anaichezea Ureno amepangwa kundi moja kuvaana na Hispania ambapo kuna marafiki zake wengi wa Real Madrid.

Makundi yalivyopangwa haya hapa.

FIFA WORLD CUP 2018 Draw

Group A: Urusi, Saudi Arabia, Misri, Uruguay

Group B: Ureno, Hispania, Morocco, Iran

Group C: France, Australia, Peru, Denmark

Group D: Argentina, Iceland, Croatia, Nigeria

Group E: Brazil, Switzerland, Costa Rica, Serbia

Group F: Ujerumani, Mexico, Sweden, Korea Kusini

Group G: Ubelgiji, Panama, Tunisia, England

Group H: Poland, Senegal, Colombia, Japan

Leave a Comment