×

Msikiti wa Kisasa Kujengwa Chanika

Wakionyesha ramani ya msikiti huo utakavyokuwa.
Mwakilishi wa ujenzi huo wa msikiti wa kisasa, Nasr Al Jahadhamy (katikati) akizungumza na waandishi wa habari.
gg
Kutoka kushoto ni hekhe, Nadir Mahfoudh wa wa Al- Noor Charitable AgencyNasr Al Jahadhamy na Sheikh  Sultan Alriyamy.
Nasr Al Jahadhamy (kushoto) akionesha waandishi wa habari sehemu utaonjengwa msikiti huo. Hawapo pichani.
Wakiendelea kutazama sehemu ambayo msikiti huo utajengwa ambao unatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka huu.

MWAKILISHI wa Masjid Rahman kutoka nchini Oman, Nasr Al Jahadhamy, amesema kuwa atajenga msikiti mkubwa katika eneo la Zingiziwa-Chanika nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam ambao utabeba zaidi ya watu 500.

 

Hayo ameyasema leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameelezea malengo yake kuwa ni kuwasaidia wananchi hasa ambao wapo pembezoni mwa mji ambao wanahangaika kupata sehemu ya kufanyia ibada.

 

Amesema kuwa msikiti huo utakuwa wa kisasa kwani utakuwa na sehemu ya kuoshea maiti, nyumba ya imamu, madrasa na sehemu ya maduka kwa ajili ya huduma mbalimbali.

 

Kwa upande wake Shekhe, Nadir Mahfoudh wa Mskikiti wa Al- Noor Charitable Agency, ameelezea kuwa kuwepo kwa msikiti huo katika eno hilo ni jambo la heri kwani waumini wa Dini ya Kiislamu ambao wamekuwa wakihangaika kutoka eneo hilo kwenda sehemu nyingine kufanya ibada, itawarahisishia kupata huduma ya kuabudu kwa urahisi.