×

A.K.A Za Dalali Acha Kabisa!

Hassan Dalali.

UKIZUNGUMZIA soka la Tanzania ni ngumu kuzikwepa kla­bu kongwe za Simba na Yanga ambazo zinaongoza kwa kuwa na mashabiki wengi ku­liko timu nyingine zinazoshiriki Ligi Kuu Bara.

 

Kwa upande wa viongozi wa soka, jina la Hassan Dalali nalo ni maarufu kutokana na kujijengea heshima kwenye mchezo huo alipokuwa kion­gozi wa Simba.

 

Dalali ni mmoja kati ya wale wazee wa zamani wa Msim­bazi, aliyeshika nyadhifa kadhaa kab­la ya kuwa kiongozi wa juu wa Sim­ba. Anafahamika kuwa ni mwenye mapenzi ya kweli na klabu hiyo.

 

Anajulikana kwa kutokuwa na makuu, lakini mwenye mipango na huenda alikuwa akidharaulika kwa kigezo kwamba hajaenda shule kwa kiwango cha kuitwa msomi kabla ya hivi karibuni kuamua kurejea daras­ani kupiga kitabu upya lakini ameba­rikiwa hekima na busara.

 

Mara zote kiongozi huyo ame­kuwa mtu wa watu, ukipata bahati ya kupiga naye stori za hapa na pale utagundua jambo hilo, ni mcheshi, anapenda utani kwani kuna ma­jina amepachikwa na mwenyewe anayafurahia.

Championi Ijumaa linakucham­bulia majina hayo katika makala haya ambayo amekuwa aki­itwa kiongozi huyo na wadau mbalimbali wa Simba na mch­ezo wa soka hapa nchini huku mengine akijipa mwenyewe:

FIELD MARSHAL (FM)

Maana halisi ya jina hili ni cheo cha mwisho au cha juu kabisa katika jeshi. Mashabiki wa Simba wal­impa jina hilo kutokana na kumuona ni kiongozi shupavu, anakumbukwa kwa kuiwezesha klabu hiyo kununua eneo li­nalotarajiwa kujengwa uwanja wa mazoezi lililopo Bunju nje ki­dogo ya Jiji la Dar.

Mashabiki wa Sim­ba wameendelea kumuita jina hilo wakati wote na mwenyewe amekuwa akilifurahia kutokana na heshima aliyojijengea kwenye timu hiyo kuanzia 2006 hadi 2010 alipokuwa mwenyekiti kwenye klabu.

 

HANDSOME BOY (HB)

Kwa lugha rahisi maana yake ni mvulana mtanashati am­baye wakati wote anakuwa kwenye mwonekano nadhifu, hivyo ndivyo ilivyo kwa Dalali ambaye mara nyingi hupenda kutupia kanzu yake nyeupe, koti na kibalaghashia.

Licha ya umri wake kuwa mkubwa mwenyewe anap­enda kuitwa kwa jina hilo la Handsome Boy au HB kama anavyoitwa na mashabiki wa timu hiyo kutokana na mwonekano wake ikizingatiwa hivi karibuni amemaliza elimu yake ya kidato cha nne.

TRUMP

Anakumbukwa na wengi kwa kuwa enzi zake akiwa mwenyekiti wa Simba alikuwa akiinyanyasa Yanga ambao ni wapinzani wakubwa wa Simba.

Dalali akiwa kiongozi wa Sim­ba alikuwa akiifunga Yanga mara nyingi kasoro mwaka 2008 ambapo Benard Mwalala alifunga bao lililoipa ush­indi timu hiyo ya Jangwani.

Mashabiki wa Simba wanamfa­nanisha kiongozi wao huyo wa zam­ani na rais wa sasa wa Marekani am­baye ni rais wa 45 katika taifa hilo, Donald Trump, sababu kubwa wote ni watu wa misima­mo mikali.

S a b a b u nyingine ya m a s h a b i k i wa timu hiyo kumpachika jina hilo ni kutokana na kiongozi huyo kuamini katika kusi­mamia jambo la kweli na lenye maendeleo kama ilivyo kwa Trump mwenyewe anayepinga matumizi ya nguvu za nyuklia.

KIM JONG-UN

Mashabiki wa Simba wanadai wakati wa utawala wa Dalali ndani ya timu hiyo alikuwa mtata hasa dhidi ya watani zao Yanga, wakaona siyo kesi wakaamua kumpachika jina la Rais Korea Kaskazini, Kim Jong-un.

Dalali mwenyewe ana­tajwa kuwa mmoja wa vi­ongozi waliowahi kutokea kwenye timu hiyo wakiwa wenye msimamo mkali kama ilivyokuwa sasa kwa rais wa Korea Kaskazini ambaye ni mtoto katika uzao wa Kim Jog-il (rais wa pili wa Korea Kaskazini) na kwa sasa ndiye kiongozi wa nchi hiyo, alichukua cheo hicho baada ya kifo cha baba yake, Desemba 2011.

DALALI MWENYEWE HUYU HAPA:

Alipoulizwa Dalali kuhu­su majina hayo alikiri kuyatambua na kusema hawezi kuyakataa kwa kuwa ni sehemu ya mchezo anaoupenda wa soka.

“Ni majina ambayo nakutana nayo kila siku, naitwa jina fulani kutegemea na eneo nililopo lakini kwangu hayana tatizo na ninay­akubali tu,” anasema.