×

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MWANASHERIA MKUU, NAIBU WAKE LEO IKULU, DAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya, Dkt. Adelardus Kilangi Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Paul Joel Ngwembe Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha, Mhe. Gerson J. Mdemu kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaangalia wakila kiapo cha maadili ya viongozi kutoka kulia ma-Jaji wa Mahakama kuu Mhe. George Mcheche Masaju na Mhe. Gerson J. Mdemu, wakifuatiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya Dkt. Adelardus Kilangi na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Paul Joel Ngwembe baada ya kuwaapisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018

Rais Magufuli leo amemwapisha Dk Adelardus Kilangi  kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Paul Ngwembe kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

 

Kabla ya uteuzi, Dk Kilangi alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (St.Augustine University) kampasi ya Arusha, pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta, (Tanzania Petroleum Upstream Regulatory Authority- PURA).

 

Naibu Mwanasheria Mkuu Paul Ngwembe kabla ya uteuzi, alikuwa Mkurugenzi wa masuala ya sheria katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (Tanzania Insurance Regulatory Authority-TIRA).

 

Wateule wote wanatarajiwa kuapishwa Jumamosi asubuhi tarehe 3 Februari 2018.

Awali katika maadhimisho ya Siku ya Sheria, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli katika hotuba yake, aliwanyooshea vidole Waziri wa Katiba na Sheria, Prof Palamagamba Kabudi, na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju na Naibu wake Gerson Mdemu wameshindwa kuandaa kanuni za msaada wa kisheria.