×

Breaking News: Moto Waunguza Shule ya Wasichana Korogwe

Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe  iliyoko wilayani Korogwe Mkoa wa Tanga, inaungua moto usiku huu, huku chanzo cha ajali ya moto huo kikiwa hakijajulikana.

Inadaiwa watu kadhaa wamejeruhiwa kutokana na moto huo. Hakuna vifo vilivyoripotiwa ama kuthibitishwa hadi sasa.

Tunaendelea kufuatilia kwa kina, taarifa zaidi tutakuletea baadaye.

Updates

Mabweni mawili ya Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe yameteketea kwa moto usiku wa kuamkia.

Moto huo ulianza majira ya saa 3 usiku, huku wanafunzi wote walikuwa madarasani (preparation) maarufu kama prepo.

Majeruhi takribani 15 wa tukio hilo hiyo walitokana mshtuko wa moyo lakini walikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Magunga na wanaendelea vizuri.