Dak Ya 90 Mpira umemalizika Uwanja wa Taifa Simba SC 2-2 Al Masry
Dak ya 73, Gooooooli, Okwi anafunga bao la pili, sasa ni 2-2
Dak ya 64, Kotei anapasi kwake Gyan, Gyan kwake Okwi, Okwiiii inagonga mwamba, hatari
Dak ya 60, Free Kiki inapigwa kuelekea Masry, Kichuya anapiga, anapigaaa, kipa anadaka
Dak ya 56, Kapombe anapoteza mpira kizembe, Masry wanachukua, Nyoni anapewa kadi ya njano baada ya kucheza madhambi
Dak ya 55, Hatariiii katika lango la Masry, mpira unapita na kwenda nje
Dak ya 47, unapigwa kuelekea lango la Simba, Manula anadaka, anaanza taratibu na mabeki zake
Dak ya 52, Kwasi ameumia, mpira umesimama
Kipindi cha pili kimeanza, Simba wanashambulia kwa kasi
Mechi ni mapumziko wenyeji Simba wakiwa nyuma na wageni Al Masry wakiongoza.
Simba SC 1 – 2 Al Masry Bocco 10′ (P) Ahmed 11′ Abdalrauf 26′ (P)
Dak ya 47, Masry wanatumia muda mwingi kupoteza muda
Dak 3 zimeogezwa na Shiza Kichuya anapewa kadi ya njano
Dak ya 42, Simba wanapata kona, inapigwa, lakini mpira unatoka nje, ni goli kiki
Dak ya 41, Hatari katika lango la Simba lakini mabeki wanaokoa, mpira unapigwa mbele na mabeki wa Masry wanatoa, unarushwa kuelekea Masry
Dak ya 40, Matokeo bado ni 2-1
Dak ya 36, Mpira umeshaanza, sasa Nyoni kwake Kichuya, unapigwa kwake Kotei, faulo.
Dak ya 29, Faulo inatokea hapa baada ya Kotei kudondoshwa, Kapombe sasa anamtafuta Okwi lakini mpira unaokolewa na wapinzani
Dak ya 27, Mchezaji wa Masry amedondoka hapa, Masry wako mbele kwa mabao 2-1
Dak ya 25, Gooooo, Masry wanafunga la pili, penati ya Ahmed inaingia kimiani
Dak ya 18, Mpira anao Asante Kwasi anampigia Bocco lakini unaokolewa, Simba wanauchukua tena kwake Okwi, mabeki wa Masry wanambana na kumnyang’anya mpira
Dak ya 12, Simba wanapasiana sasa eneo la nyuma, Kapombe anampasia Kapombe, Kapombe kwake Erasto Nyoni
Dak ya 11, Gooooooli, Masry wanasawazisha hapa ni 1-1, mfungaji ni Mohammed Gomaa
Dak ya 9, Bocco anapigaaa, gooooooooooooooli
Dak ya 8, Penatiiii, Simba wanapata penati baada ya beki wa Masry kuushika mpira
Dak ya 6, Hatari katika lango la Masry, Nyoni anapiga krosi, kona, Kichuya anapiga tena kipa anaokoa na kuutoa nje, kona ya pili
Dak ya 4, Masry wanaanza sasa, unapigwa mreefu mpaka kwa kipa wa Simba, Manula anaudaka
Dak ya 3, Okwi anakwenda mpira pembezoni kuli mwa Uwanja, anapiga krosi lakini unaokolewa hapa
Dak ya 2 Al Masry wanakosa bao la wazi kipa wa simba anatoa nje ya uwanja
Dak ya 1, Mechi imeanza katika Uwanja wa taifa